Mmi ni mwandishi wa habari naitwa Stella Ibengwe naandikia gazeti la Tanzania Daima napatikana Mkoa wa Shinyanga.
kazi hii ya uandishi wa habari niliianza mwaka 2006 baada ya kumaliza chuo cha uandishi wa habari na utalii Musoma mwaka 2005.nawakaribisha sana katika taaluma hii kwani ni nzuri inakufanya ufahamiane na watu wengi wa aina zote kimataifa na dunia nzima pia inakuwezesha kufahamu mambo mengi yanayoendelea hapa nchini na duniani kote.
Mimi kama mwandishi wa habari taaluma yangu inaniwezesha kutembelea maeneo ya vijijini na mijini ili kupata taarifa zinazowahusu wakazi wa vijijini ikiwa ni pamoja na changamoto zinazowakabili na hatimaye kuzipatia ufumbuzi kwa kuwafikia viongozi husika.
Na pia tutambue kuwa katika taifa letu kuna wimbi kubwa la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino pamoja na vikongwe hivyo mimi kama mwandishi ninawajibu wa kuihamasisha jamii iondokane na imani potofu ya kuwauwa vikongwe na albino kutokana na imani za kishirikina,
baada ya kusema hayo napenda niishie hapa na watakia kazi njema katika ujenzi wa taifa.
No comments:
Post a Comment