Wednesday, October 28, 2009

Stella Ibengwe

Naitwa Stella Ibengwe, ni mshiriki wa mafunzo ya huduma ya kutumia mtandao wa Internet yanayotolewa na Misa –Tanzania kwa kushirikiana na VIKES Foundation kwa waandishi wa habari 20 kutoka mikoa minne ya kanda ya ziwa ambayo ni Mwanza,Shinyanga,Mara na Kagera.

Mimi pia ni mwandishi wa habari niko kampuni ya Freemedia inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari. Mafunzo haya ni mazuri kwa mwezeshaji anafundisha vizuri washiriki tunamuelewa na pia tunauliza maswali na kupatiwa ufafanuzi panapohitajika.

Mafunzo haya tulianza kufundishwa Oct 26 ambapo yataendelea hadi Oct 30 mwaka huu na leo tumejifunza jinsi ya kutumia mtandao wa internet kama mwandishi wa habari ikiwa ni pamoja na jinsi ya kufungua web site ambapo tayari washiriki wote wamefauru kwa zoezi hilo lililofanyika chini ya mkufunzi wetu Peik Johansson. Kupitia mtandao wa internet utatuwezesha kupata taarifa mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi pamoja na kuwasiliana na ndugu,jamaa na marafiki.

Tunashukuru mafunzo haya yanaendelea vizuri na ninaimani yatamalizika vyema na kila mmoja wetu atakuwa ni mwalimu mzuri kwa waandishi wengine ambao hawakupata nafasi ya kushiriki pia hata jamii nzima.

No comments:

Post a Comment